MSANII JB ATANGAZA KUSTAAFU KUIGIZA FILAMU.
Akiongea na waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam wakati akitambulisha rasmi filamu yake ya "KALAMBATI LOBO" ambayo ameshirikiana na msanii maarufu Diana kimaro,Jb amesema kwa sasa anaandaa filamu nyingine baada ya hii na itakapokamilika na kuzinduliwa ndipo ataachana kabisa na kuigiza na kuanza kutayarisha na kuongoza filamu za wasanii wengine.
"Kama nilivyokuwa natangaza kukaribia kustaafu kuigiza,ili napenda niliweke wazi kuwa baada ya kalambati lobo nitatoa filamu yangu ya mwisho ambayo bado nagombana na distributers itoke tarehe 31 na baada ya hapo nitakuwa nyuma ya kamera kuwa kama producer na Director hivyo nitaachana kabisa na uigizaji" alisema Jb.
Msanii JB,katikati akizungumza na waandishi wa habari juu ya kustaafu kwake pindi alipokuwa akitambulisha filamu yake mpya ya "KALAMBATI LOBO "katika ukumbi wa Idara ya habari maelezo Jijini Dar es salaam.
Aidha,Msanii huyo amesema ameshafanya filamu zaidi ya 40 kupitia kampuni ya jerusalemu na watanzania wamekuwa wakimuunga mkono hivyo anawaomba waendelee hivyo hivyo kwa hizi filamu mbili zilizobakia kabla ya yeye kustaafu.
Baadhi ya waandishi wa habari wakichukua taarifa juu ya tukio hilo la kutambulishwa kwa filamu yake hiyo.
Hata hivyo msanii huyo aliweza kuwashauri wasanii wachanga ambao hawajapata fursa ya kufahamika na wangetaka wasaidiwe,amesema kuwa njia rahisi ni kujiunga katika vikundi mbali mbali vya sanaa ili waweze kuonekana kupitia tamthilia ama kushiriki katika mashindano mbali mbali yanayoandaliwa na makampuni tofauti wapate kujulikana kwa sababu kampuni yake ya jerusalemu haitaweza kuwafikia wasanii wote na hata gharama za utayarishaji wa kampuni yake itakuwa juu sana hivyo njia ya kuwasaidia hao ni kushiriki kwenye mashindano hayo ama kujiunga na vikundi hivyo
Leave a Comment