WANASAYANSI WATABILI KUPATWA KWA JUA KIPETE
Wanasayansi kutoka chuo kikuu huria Tanzania wamethibitisha
kuwapo kwa tukio la kupatwa kwa jua kipete mwezi septemba kwenye usawa wa nchi
yetu hasa maeneo ya kusini na jirani.
Mtaalam wa Astronomia na Mhadhiri wa fizikia kitivo cha
sayansi,Teknolojia na Elimu ya Mazingira Chuo kikuu huria Dr. Noorali jiwaji
ameeleza tukio hilo kuwa ni la kihistoria na hutokea kwa nadla sana maana jua
huonekana kama pete badala ya mviringo.
Dr.Noorali kushoto akionyesha sampuli ya chujio maalumu ya mwanga na pembeni yake ni makamu mkuu wa chuo kikuu huria Tanzania Prof.Elifas Bisanda.
Dr Noorali amesema , tarehe 1 septemba ,kuanzia saa 4 asubuhi
hadi 8 alasiri ,wakazi wa Rujewa kusini mwa Tanzania, karibu na Mbeya
watashuhudia duara la jua linavyobadilika kuwa pete ya jua huku watanzania kote
nchini wataona jua kali la utosini likimegwa kwa Zaidi ya 90% kwa kufunikwa na
mwezi na kuliacha jua lionekane kama hilali nyembamba au kama mwezi mwandamo.
“Tarehe 1 septemba,Watanzania wanaoishi mikoa ya kusini
wataona jua kama pete kwa dakika chache, wakati Tanzania kote pamoja na wa
kusini wataona jua limepatwa kihilali kwa masaa manne”alisema.
Aidha, ametaja maeneo mengine ya kusini ambayo jua litapatwa
kipete kuwa ni Katavi,Rukwa,Mbeya,Njombe,Ruvuma na Mtwara na sehemu zote za
Afrika na Madagaska,huku akiwataka watu kutumia chujio maalum ya mwanga ili
kuepuka madhara ya mionzi ya jua kama wataangalia
moja kwa moja au kutumia vifaa vingine vya kiza vilivyotengenezwa kienyeji, huku
akisifu jitihada za kampuni ya SBC kwa kuahidi kudhamini vichujio 50,000 vya
mwanga vitavyosambazwa mashuleni.
Hii si mara ya kwanza kutokea kwa tukio hili nchini
kwani julai 31, 1962, miaka 54 iliyopita , April 18, 1977 miaka 33 iliyopita na likipita
litatokea tena mei 21, 2031 miaka 15 ijayo na feb 17, 2064 baada ya miaka 48,
hivyo ni tukio la kihistoria na la kujifunza kwa wanafunzi wanaopenda masomo ya
sayansi.
Leave a Comment