KAMPUNI YA HALOTEL YATOA MSAADA WA MADAWATI KWA WANAFUNZI WA MKOA WA TABORA.

Pichani ni Ngo Duy Truong ambaye ni Meneja masoko wa Kampuni ya Halotel wa kwanza kushoto,na kati kati ni Dr.Amon Mkoga,mwenyekiti wa taasisi ya Dr.Amon Mkoga na wa mwisho kulia ni Stella Pius ambaye ni Afisa Masoko wa Halotel wakionyesha picha ya kampeni ya SIMAMA KAA DESK CAMPAIGN.

Kampuni ya mtandao wa simu za mkononi ya Halotel hapa nchini kupitia Taasisi ya Dr.Amon Mkoga imetoa msaada wa madawati kwa wanafunzi wa Mkoa wa Tabora ili kupunguza chanagamoto za kielimu zinazowakabili. 

Akitoa taarifa hiyo leo kwenye ukumbi wa Idara ya Habari Maelezo, Jijini Dar es salaam,Afisa Mawasiliano wa Kampuni hiyo, Bi. Stella Pius, amesema wameamua kusaidia madawati hayo kutokana na changamoto zinazozikabili shule nyingi za mkoani humo.
 

Aidha,Bi.stella amesema mpango huo ni kuunga mkono wito wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dr.John Pombe Magufuli, katika kupunguza uhaba wa madawati nchini.
Bi. Stella pius akiongea na waandishi wa habari juu ya sababu za wao kusaidia kutoa madawati hayo kupitia kampeni hiyo.

"Halotel ikishirikiana na Foundation ya Dr. Amon Mkoga tumeamua kushirikiana katika suala la kampeni hii ya" SIMAMA KAA DESK CAMPAIGN" ikiwa ni mojawapo ya muitikio wa kampuni yetu ili kuitikia wito wa Mh.Rais john Pombe magufuli katika kupunguza uhaba wa madawati mashuleni kwa sababu ukiangalia kwa kiasi kikubwa shule nyingi mikoani zina uhaba wa madawati kwa asilimia kubwa"alisema Bi stella.
 

Nae Mwenyekiti wa Foundation hiyo Dr.Amon Mkoga amesema Taasisi yake kupitia kampeni ya "SIMAMA KAA DESK CAMPAIGN" ina lengo la kupunguza uhaba wa madawati katika mkoa wa Tabora ili kuweza kutatua changamoto za kielimu katika maeneo ya vijijini.

Mwenyekiti wa Taasisi hiyo  Dr.Amon mkoga akizungumzia juu ya kazi zinazofanywa na Taasisi yake huku akiwashukuru wadhamini hao ambao wamesaidia kufanikishwa kwa zoezi hilo ambalo limeanzishwa na Taasisi yake.

"Sisi kama Dr. Aman mkoga Foundation kazi yetu kubwa tunapokea maombi mbali mbali kutoka katika wilaya ambazo hazijafikia kiwango cha asilimia mia kwa mia hasa katika upande wa madawati, hivyo tunashawishi wadau mbali mbali ili tuweze kushirikiana nao katika utatuzi wa changamoto hizo"alisema Dr.Mkoga. 
Baadhi ya wana habari ambao waliudhulia tukio hilo katika ukumbi wa habari maelezo Jijini Dar es salaam.
Taasisi ya Dr Amon Mkoga inafanya kazi za elimu katika mikoa miwili ya Pwani na Tabora na kwa sasa imeanzisha kampeni yenye lengo la kutatua changamoto za elimu kwa kuzisaidia jamii hizo kupitia maombi ya kutoka katika maeneo yanayokabiliwa na changamoto hizo nao kutafuta wahisani ili kusaidia.
 

Hata hivyo kupitia kampeni hiyo tayari shule 4 kutoka Tabora zimeshafaidika na madawati 400 yameshawafikia wahusika na mengine 200 yameshaandaliwa ili kuwapelekea viongozi wa wilaya ili wajue wayapeleke shule gani madawati hayo.

No comments

Powered by Blogger.