WAZIRI:WASICHANA HATUTAWAACHA NYUMA.




Waziri wa Afya mhe.Ummy Mwalimu amesema serikali haitawaacha nyuma wanawake katika masuala ya maendeleo kupitia mpango wake uliojiwekea katika serikali ya awamu hii.

Waziri ummy ameyasema hayo akiwa katika uzinduzi wa siku ya idadi ya watu duniani ambayo imehadhimishwa leo tarehe 11,juni 2016,katika viwanja vya mnazi mmoja jijini Dar es salaam ikiwa na kauli mbiu ya "wezesha msichana afikie ndoto zake".

Tutapita nyumba hadi nyumba,kata hadi kata,mkoa hadi mkoa katika kutekeleza mpango wa maendeleo hasa ukizingatia serikali hii ni ya uchumi wa viwanda na mimi niseme wasichana hatutawaacha nyuma.alisema.

 Aidha,amesema kumekuwa na changamoto kubwa za ukatili wa kingono na elimu kwa wasichana ambazo zimebainishwa kupitia tafiti za kitaifa za mwaka 2011 kwa kushirikiana na UNICEF, huku akitolea mfano katika uwiano wa elimu kwa wavulana kuwa juu tofauti na wasichana hasa kwa elimu ya juu, licha ya kufanana katika elimu ya msingi.

Mwakilishi kutoka UNFPA Bi.Natalia kanem akitoa hotuba yake katika siku hii ya uzinduzi wa Siku ya idadi ya watu duniani huku akiahidi kuhadhimishwa kila mwaka kutokana na makubaliano ya nchi uanachama wa UNFPA ili kuhakikisha msichana anatimiza ndoto zake.




Waziri wa Afya Bi.Ummy Mwalimu (kulia) akiwa na mwakilishi kutoka UNFPA Bi Natalia Kanem (kushoto) wakiwa wameshika picha iliyoandikwa kauli mbiu ya uzinduzi wa siku ya idadi ya watu duniani.

Waziri wa Afya Ummy Mwalimu ( kushoto) akipokea kitabu toka kwa mwakilishi wa TAMWA ambao nao walishiliki katika maadhimisho hayo.

No comments

Powered by Blogger.