ASKARI POLISI WAUWAWA DAR,NCHEMBA AWATAKA WALIOHUSIKA KUJISALIMISHA.
TUNAOMBA RADHI KWA BAADHI YA PICHA UTAKAZOZIONA.


ASKARI polisi 4 wameuawa kwa kupigwa risasi na majambazi huko Mbagala, mbande jijini Dar es Salaam usiku wa kuamkia leo.
Inadaiwa kuwa askari hao walikuwa
wakibadilishana lindo katika Benki ya CRDB, tawi la Mbagala mbande na
mara wakaibuka watu wanaodhaniwa kuwa ni majambazi na kuanza
kuwashambulia kwa risasi na baada ya shambulizi hilo wanadaiwa kuondoka
na pikipiki wakielekea maeneo ya Mvuti.
Polisi waliouawa ni pamoja na;
E5761 CPL YAHAYA
F4660 CPL HATIBU
G9544 PC TTITO.
Inasemekana kuwa tukio hilo limetokea
mnamo saa 1: 30 usiku katika na inadaiwa kuwa wahalifu hao waliondoka na
silaha moja aina ya SMG.
Mmoja kati ya polisi waliouawa alikuwa
anaingia lindo, mmoja alikuwa anatoka na mwingine alikuwa dereva na
imeelezwa kuwa majambazi hayo hayakuingia ndani ya benki ila gari la
polisi (Leyland Ashok) limeharibiwa kwa risasi.
Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es
Salaam, Simon Sirro amethibitisha kutokea kwa tukio hilo: “Ni kweli
kumetokea tukio la uvamizi hapa Mbagala lakini taarifa kamili nitazitoa
kesho kwa kuwa bado nipo eneo la tukio kwa ajili ya uchunguzi zaidi”.
Alisema Kamanda Sirro.
"Usiku huu nimefika Mbande-Temeke,eneo
lilipofanyika tukio baya la uhalifu wa kutumia silaha ambapo
watu/majambazi zaidi ya saba wakiwa na silaha wamevamia eneo la Benki ya
CRDB-Mbande na kuua askari 4 waliokuwa wakishuka kwenye gari tayari
kwa kupokezana lindo.
Pia wamejeruhi raia wa kawaida wawili,nimewajulia hali zao na wote wanaendelea vizuri.
Hatutaishia
kulaani tu tukio hili na matukio mengine kama haya,natoa rai kwa
wahusika kujisalimisha.Vilevile wananchi na raia wema tunaomba
ushirikiano wenu katika vita hii ya kupambana na wahalifu hawa na
wanaotuzunguka kwenye maeneo yetu."
Mwigulu Nchemba
Leave a Comment