PPF KUENDELEA KUHAKIKI WASTAAFU,WAJA NA WOTE SCHEME.
Meneja uhusiano wa PPF, Bi.Lulu Mengele akiuelezea mfumo huo wa "WOTE SCHEME" ambao unahusisha makundi yote ya wazalishaji yaani wakulima,wajasiriamali na wavuvi ambapo wataweza kuchangia mahala popote kupitia simu za mkononi baada ya kuwa wamejiunga kupitia mifumo ya computer.
Mfuko wa hifadhi ya jamii wa PPF umewatarifu wanachama wake juu ya muendelezo wa zoezi la kuhakiki wastaafu wao ili kuwa na kumbu kumbu sahihi za wastaafu ambao wanawalipa penshion kila mwezi.
Akitoa taarifa hiyo jana katika ukumbi wa Idara ya Habari Maelezo Jijini Dar es salaam,Meneja Kiongozi wa Huduma za Pensheni ,Bw.John Mwalisu amesema zoezi hilo limekwisha anza tangu tarehe 12 septemba na kukamilika jana tareh23 katika mikoa 3 ambayo ni Dar es Salaam,Pwani,Tanga na visiwani Zanzibar.
Meneja amesema kuwa wamekuwa na utaratibu wa kuhakiki wastaafu kila baada ya miaka miwili ili kuwa kumbu kumbu sahihi juu ya wastaafu hao na zoezi hili ni endelevu hivyo kwa wale wasiopata nafasi hiyo wasitie shaka kwani watahakikiwa kama kawaida.
“Lengo la kuhakiki ni kuwa na kumbu kumbu sahihi za wastaafu tunaowalipa kila mwezi maana hili ni daftari na kuna watu wamebadili maeneo wanayoishi ama sehemu ya kuchukulia pesa hivyo zoezi hili ni kutaka kuoanisha taarifa zao ili tusije kumpa mtu pesa ambaye hastahlii.alisema meneja kiongozi.
Aidha Mwalisu ameitaja mikoa mingine ambayo sasa zoezi linatarajiwa kuenda kuanza kuwa ni Morogoro,Arusha ,mwanza na mbeya na linatarajiwa kuisha tarehe 28 octoba mwaka huu.
Leave a Comment