ALIYEMPONGEZA MAGUFULI HADHARANI APATA SHAVU.
Kijana mmoja mkazi wa Dar es salaam amepata nafasi ya kupiga picha na Mhe. Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Dr.John Pombe Magufuli baada ya kumsifu hadharani na kumpongeza kwa kazi kubwa anayofanya muheshimiwa rais.
Kijana huyo aliyefahamika kwa jina la Omary Abdallah Ramadhani amefanya tukio hilo alipokutana na rais katika viwanja vya maonyesho ya Saba Saba jijini Dar es salaam siku ya ufunguzi uliohudhuriwa na wageni mbali mbali wakiwemo viongozi wa nchi,wake wa marais na mgeni rasmi ambaye ni Mhe.Paul Kagame wa Rais wa Rwanda.
Rais magufuli ambaye aliongozana na mke wake Mama Janeth Magufuli aliweza kutembelea baadhi ya mabanda yaliyopo viwanjani hapo huku akilakiwa na mamia ya wananchi waliokuwa na hamu ya kumuona akiwemo Bw.Omary ambaye uvumilivu ulimshinda na kupiga kelele hadharani za kumpongeza mheshimiwa rais.
Kijana Omary kushto akiwa na Mhe.Dr.magufuli katikati na mke wa Rais kulia mama Janeth Magufuli wakati wakipiga picha.
Kijana Omary kulia akiwa na mwandishi wa habari wakati wa mahojiano.
Kijana Omary kati kati akiwa anaelezea sababu za yeye kujiamini hadi kumpongeza mheshimwa rais hadharani.
Mheshimiwa Mkuu wa mkoa Paul Makonda akiongea jambo na baadhi ya watu waliomzunguka.
Mheshimiwa Rais Dr.Magufuli akiwa na Mheshimiwa Paul kagame kulia baada ya kutembelea baadhi ya mabanda yaliyopo viwanjani hapo.
Mheshimiwa Rais Dr.Magufuli kushoto akiwa na Mh.Paul Kagame wakitoka nje ya ofisi za Tantrade baada ya kumaliza ziara yao katika viwanja vya Saba Saba.
Mheshimiwa Rais Dr. Magufuli akifulahi jambo na mkewe mama Janeth magufuli.
Wananchi waliojitokeza kumtazama Rais pindi alipotembelea viwanja vya Saba Saba jijini Dar es salaam wakati wa siku ya ufunguzi.
Baadhi ya wanachi waliopata nafasi ya kutembelea maonyesho hayo wakimtazama Rais wa nchi huku jeshi la polisi likiweka ulinzi wa kutosha viwanjani hapo.
Leave a Comment