KANALI MSTAAFU ATUMIA MANENO YA NYERERE KUONGEA NA WANASIASA UCHWARA


Kanali mstaafu(kushoto) ametumia maneno ya kitabu cha mwalimu nyerere "Tujisahihishe" ili kuongea na wanasiasa uchwara juu ya ubinafsi.

Akiongea na waandishi wa habari katika ukumbi wa habari maelezo,Kanali Dkt.Haruni Ramadhani Kondo amesema wanasiasa uchwara hivi sasa kazi yao kubwa imekuwa kupandikiza mbegu za fitina,chuki na husuda miongoni mwa wananchi ili kuleta vurugu,uhasama na hata vita,watu hao hawajali wala hawana mapenzi ya nchi yao,watu hawa ni mabingwa wa kukejeli,kudharau,kubeza na kudhalilisha kila kitu na kudai hakuna jema,yote ni mabaya.

Akitumia maneno ya kitabu hicho kilichoandikwa mei 1962 na Baba wa taifa,mwalimu jk Nyerere,Dkt Kondo amesema kitabu hicho kilikuwa kinawaonya viongozi na wananchi wake juu ya madhara ya ubinafsi kwa nchi changa kama Tanzania iliyodhamiria kujenga demokrasia na kuleta maendeleo ya wananchi wake.

"Mwalimu nyerere ameandika katika kitabu hicho kuwa ukweli una tabia ya kijilipiza kisasi ukipuuzwa,Mwalimu amesema mtu anaweza kuamua kulipiga teke jiwe,lakini watu wenye busara watamwonya kuwa hilo sio dongo ni jiwe kwa ukahidi,kibri na dharau mtu huyo akapuuza ushauri huo akaendelea na uamuzi wake akalipiga teke hilo jiwe,mwalimu anasema mtu huyo atavunja dole ama mguu.ukweli haupendi kupuuzwa"alisema
Aidha,amesema kitabu hicho kidogo chenye hazina kubwa ya busara na hekima,Mwalimu anapinga na kukosoa tabia ya ubinafsi iliyojitokeza miongoni mwa viongozi na wananchi ambayo mwalimu aliiona ni hatari na adui mkubwa wa umoja na mshikamano kwa ustawi wa nchi.

"Mitazamo na hoja hiyo ya Baba wa taifa bado ni hai na yenye mantiki kubwa hivi sasa katka demokrasia ya mfumo wa vyama vingi kuliko wakati ule"alisema

Pia,aliwahasa wananchi kukataa hadaa na propaganda za wanasiasa uchwara kwani ubinafsi uliokubuhu unapelekea kubomoa misingi ya mshikamano na umoja wa taifa letu,pia ni ugonjwa uliokumba kada zote hususani wanasiasa kutokana na uchu na uroho wa madaraka watu hao bila aibu ama uoga wamekuwa wakipita huku na huko kupandikiza mbegu za chuki,fitina miongoni mwa wananchi ili kutimiza malengo yao,nchi nyingi zimeingia kwenye migogoro,vurugu na vita vya wenyewe kwa wenyewe kutokana na maradhi au gonjwa hilo ambalo sana limepelekea hasadi/husuda.

"Watanzania tunapaswa kuwa makini na kukataa hadaa na propaganda za baadhi ya wanasiasa uchwara wabinafsi wenye uchu na uroho wa madaraka"alisema

No comments

Powered by Blogger.