JESHI LA POLISI LAKAMATA NYARAKA BANDIA ZA SERIKALI.

Jeshi la polisi kanda maalum ya Dar es salaam linawashikilia watuhumiwa watatu wa kesi ya kukutwa na nyaraka bandia za ofisi ya serikali.

Akiongea na waandishi wa habari jijini Dar es salaam Kamishna wa Polisi kanda maalumu Simon.N.Sirro amesema walipokea taarifa kutoka kwa raia wema kuwa huko buguruni Ghana kuna watu wanajihusisha na vitendo vya kiuhalifu na uuzaji wa madawa ya kulevya na baada ya kuwakamata na kuwapekua katika nyumba wanayoishi ndipo walikuta nyaraka hizo bandia za serikali.

Aliwataja majina ya watuhumiwa hao kuwa ni Ashraff maumba(37)mkazi wa buguruni Ghana,Mwamba Seif(38)mkazi wa Mnyamani na Mahmudu Zuberi(24)mkazi wa buguruni,ambao wote wanakabiliwa na shitaka la kukutwa na nyaraka bandia za serikali ikiwemo vyeti vya kidato cha nne 50,stika za Sumatra 20,vyeti vya uuguzi,vyeti vya kuzaliwa 10,siri au rakili bandia za vyeti vya CBE 10,leseni za biashara,nyaraka za Bima 100
 na nyaraka za Comesa 100.

 Pia,katika tukio hilo jeshi la polisi lilifanikiwa kukamata vifaa mbali mbali vya kutengenezea nyaraka hizo zikiwemo karatasi maalum zilizo na nembo ya TRA kwajili ya kadi za vyombo vya moto 500,muhuri wa Bibi na Bwana,computer 4,printer 3,genereta na stablizer moja.
        Baadhi ya mihuri binafsi na ya serikali iliyokamatwa katika tukio hilo,ambayo hutumika kutengenezea nyaraka bandia.
        Kamishna Sirro akionyesha nyaraka za Bima walizokamata toka kwa watuhumiwa hao.
                           Mashine za printer zilizokamatwa katika tukio hilo.
Baadhi ya stika za sumatra zilizokutwa na jeshi la polisi baada ya upekuzi huo.
           Karatasi bandia zenye nembo ya TRA ambazo zimetumika kutengenezea kadi za vyombo vya moto na leseni za biashara.
       Kamishna Sirro akionyesha baadhi ya nyaraka za Comesa ambazo zilikamatwa na jeshi la polisi wakati wa upekuzi.

Watuhumiwa wote wapo kituoni na upelelezi unaendelea na utakapokamilika watafikishwa mahakamani,na wale wote waliotumia vyeti au nyaraka hizo bandia sehemu yeyote katika ofisi za serikali watatafutwa ili sheria ifate mkondo wake.
Powered by Blogger.