MOURINHO:SIKUSTAHILI KUPOTEZA MECHI DHIDI YA FEYENOORD.

Image result for MOURINHO
Kocha wa timu ya manchester united jose mourinho amesema hakustahili kupoteza mechi dhidi ya feyenoord katika ufunguzi wa europa league.

Mourinho ameyasema hayo kupitia chombo cha BT sport mjini Rotterdam ambapo timu yake ilikubali kichapo cha bao 1-0 dhidi ya wenyeji hao kupitia nyota wao tonny vilhena aliyefunga katika dakika ya 79 ambapo watu wengi wameizungumzia kama ni offside.
 

"Bila shaka mimi sina furaha Sisi kupoteza mchezo huu wakati hatukustahili  " Mourinho alisema baada ya mchezo.
 

Hata hivyo alitoa tathimini yake juu ya mchezo kwa vipindi vyote viwili huku akiisifu timu yake ilivyofanya vizuri katika kipindi cha pili lakini hawakuwa na bahati ya kushinda licha ya kupata nafasi kadhaa na hivyo kutotaka kumtupia lawama mchezaji yeyote.
 

"Kipindi cha pili  mchezo ulikuwa angalau ni mzuri ,Tulikuwa daima katika kudhibiti japokuwa walikuwa wakijaribu kushinda na si kupoteza. Ni mara mbili tumekuwa hatuna bahati kwa sababu aliefunga goli alikuwa ameotea wazi"alisema mourinho
 

Aliendelea kusisitiza kuwa "Sitaki kwenda katika upande huo. Sitaki kubinafsisha Ni wazi kuna baadhi walicheza vizuri kuliko wengine na Ilikuwa ni mchezo wao wa kwanza kwa baadhi ya wachezaji.alisema
 

katika mechi inayofuata ya manchester united kwenye Europa League, watawakaribisha Zoya Luhansk kwenye uwanja wa Old Trafford mwishoni mwa mwezi .

No comments

Powered by Blogger.