Wasanii wa Bongo fleva na movie waungana katika kuchangia wahanga wa Tetemeko la Ardhi lililotokea Bukoba mkoani Kagera.
Wakitoa taarifa hiyo leo katika ukumbi wa Idara ya Habari Maelezo jijini Dar es salaam,Viongozi wa pande zote wamesema wameguswa na mahafa hayo hivyo wameamua kuwasaidia kwa kuwachangia wahanga hao huku wakishirikiana na Kampuni ya TSN Supermarket.
Sambamba
na hilo wasanii hao wameandaa mechi ya mpira wa miguu ambayo itachezwa
siku ya Jumapili ya Tarehe 25 septemba, majira ya saa 9 katika uwanja wa
Taifa Jijini Dar es Salaam.
Msanii Steve Nyerere wa Bongo Movie, wa kwanza kulia,akiwashukuru TSN kwa kudhamini tukio hilo na Watanzania kwa ujumla waliojitokeza kuwachangia wahanga wa tetemeko la Ardhi kagera na kuwapa pole wote waliofikwa na maafa mengine kama ajali zilizojitokeza hivi karibuni huku akisema wao wameanza na hili kwakuwa wameguswa na ndio maana wameungana na wenzao wa Bongo fleva ili kuwasaidia waanga kupitia mechi hiyo itakayotoa fursa kwa Watanzaniana na makampuni mengine kushiriki kuchangia.
Mkuu wa kitengo cha Masoko na Biashara,Bw.Jahu Mohamed Kessy,wa kwanza kulia akiongea na waandishi wa Habari juu ya wao kudhamini tukio hilo na kuwataka wananchi,Mashirika na Makampuni mengine binafsi kujitokeza kwa wingi kwa ajili ya kuchangia na kuwezesha misaada kwa wananchi wa Kagera waliopata maafa kutokana na tetemeko la Ardhi.
"TSN,
yaani Tanzania sisi ni nyumbani ,tunaunganisha nguvu ya wasanii hawa
kutoka katika tasnia hizi mbili Tofauti kwa lengo la kuhamasisha
uchangiaji wa pamoja"alisema Bw.Kessy.
Nae,Msanii wa Bongo fleva nchini,Karama Masoudi a k a Kala Pina akizungumzia juu ya wao kama wasanii wa muziki kuguswa na maafa hayo yaliyosababisha hasara kubwa kwa jamii husika ,lakini ameipongeza serikali kwa jitihada wanazofanya kuhakikisaha jamii hizo zinarudi katika hali yao ya kawaida.
Pia,ameishukuru sana TSN kwa kudhamini baadhi ya vifaa ambavyo vitatumika katika mechi hiyo vikiwemo jezi,mipira na viatu kwa timu zote huku akitoa shukrani kwa mashabiki wao kwani hilo wanalofanya ni kurudisha fadhila kwa wale wote wanaounga mkono kazi zao za sanaa.
Hii si mara ya kwanza kwa wasanii hawa kuungana katika kuchangia maafa hama kuamasisha jamii juu ya maswala tofauti ambayo huwa yana lengo la kuleta matokeo chanya katika taifa.
Tazama baadhi ya picha ya picha za wasanii wengine walioudhulia tukio hilo.
Msanii wa Bongo fleva Inspekta Harouni akifurahi jambo wakati msanii mwenzie Kala pina akizungumza na waandishi wa Habari.
Mkuu wa Kitengo cha Masoko wa TSN, kulia akimkabidhi jezi msanii wa Timu ya Bongo fleva.
Mkuu wa masoko wa TSN,wapili kushoto, akikabidhi vifaa vya michezo kwa wasanii wote wa Bongo movie na Bongo fleva.
Leave a Comment