BARCELONA WASHINDWA KUTAMBA MBELE YA ATLETICO WAKIWA CAMP NOU.
Klabu ya Barcelona ya nchini hispania jana ililazimishwa sare na Atletico de Madrid ya nchini humo katika mchezo uliopigwa Camp nou.
Barcelona ambao walikuwa nyumbani katika mchezo huo waliweza kupata goli katika kipindi cha kwanza dakika ya 41 kupitia kwa Ivan Rakitic kabla ya Angel Correa kuchomoa katika dakika ya 61kwa upande wa Atletico hivyo kwenda sare ya bao 1-1 mpaka mwisho wa mchezo.
Aidha,Barcelona jana walicheza huku wakimkosa nyota wake Lionel Messi ambaye aliumia mapema kipindi cha pili na dakika ya 59 alibadilishana na Turan.
Hata hivyo usiku wa jana michezo mingine ilipigwa nchini humo ambapo Mabingwa Real Madrid nao walitoka sare ya1-1 na Villarreal,Granada 1 - 2 Athletic Bilbao,Real Sociedad 4 - 1 Las Palmas na Celta Vigo 2 - 1 Sporting Gijon.
Leave a Comment