WASANII WA MAIGIZO WAMUANGUKIA MAGUFULI JUU YA MAVAZI YA POLISI.
Katibu mkuu wa TDFAA,Ndugu jafari Mkatu ,kati kati akiongea na wana habari juu ya changamoto zinazoikabili tasnia ya uigizaji,kushoto ni msanii wa filamu maalufu kama mzee chillo na kulia ni mwenyekiti wa Chama Ndugu Ally Baucha,na nyuma ni baadhi ya waigizaji.
Chama cha waigizaji mkoa wa kinondoni kimemuomba Mh rais kupitia wizara ya Habari, sanaa utamaduni na michezo wawe na mavazi maalum yatakayoweza kuwatambulisha kama vazi maalum la kipolisi kwa wasanii wa Tanzania au msanii yoyote atakayekuja kuigiza katika ardhi ya nchi hii.
Akiongea na waandishi wa Habari jana Jijini Dar es Salaam Katibu Mkuu wa chama hicho(TDFAA) Bw.Jafari Dionizi Mkatu ameyasema hayo ikiwa ni kama sehemu ya changamoto inayowakabili waigizaji nchini pindi wanapofanya kazi zao hizo za uigizaji.
Bw.Mkatu alielezea changamoto zingine zinazowakabili katika tasnia hiyo kuwa ni eneo maalum la ardhi ambalo wataweza kufanya location za muda kwajili ya kurekodia kazi zao kama vile kutengeneza mahakama na vituo vya polisi.
"Ili Filamu na Tamthilia zetu zibebe ujumbe uliokamilika tunamuomba mh.Rais kupitia wizara ya Habari,sanaa na michezo atupatie eneo maalum la ardhi ambalo tunaweza kufanya location za muda kwa jili ya kurekodia kazi zetu kama vile kutengeneza mahakama,vituo vya polisi n.k,na wasanii wa Tanzania tuwe na mavazi maalum(uniform)yatakayoweza kututambulisha kama vazi maalum la kipolisi kwa wasanii wa Tanzania au msanii yoyote atakayekuja katika ardhi ya Tanzania".alisema katibu.
Aidha,Katibu aliiomba serikali kupitia wizara ya Habari iwaharakishie sera ya filamu ambayo itaoanisha mambo mbali mbali ya kisheria kuanzia uandaaji wa kazi,masoko,haki miliki,haki shiriki na malipo stahiki za kila kazi zao na wahusika wote ndani ya tasnia ,ulazima wa msanii kujiunga na vyama husika na kufanya kazi zenye ubora,huku akiwahasa wasanii wenzake wajiunge na Bima ya Afya kwani wasisubiri kuugua ndipo wajikite katika kuchangishana.
Mwishoni alizitaka taasisi,ngo's,sekta binafsi na serikali kuwekeza katika sanaa ili kunyanyua pato la taifa kupitia huku akizitaka Halimashauri na majiji kuwatumia wao katika shughuli mbali mbali za uzalishaji mali na matangazo ya elimu,afya,mila na destuli.
Leave a Comment