WAENDESHA BODA BODA WAGOMA KUSHIRIKI MAANDAMANO YA SEPTEMBA MOSI.

Vyama vya waendesha boda boda wa mkoa wa Dar es salaam wamepiga marufuku kwa wanachama wao kutojihusisha na maandamano ya vyama vya kisiasa vinginevyo atakae bainika atachukuliwa hatua za kisheria ngazi ya chama na hata kitaifa.

Akitoa taarifa hiyo leo ndani ya ukumbi wa Habari maelezo jijini Dar es salaam mwenyekiti wa chama cha waendesha boda boda wilaya ya kinondoni (chabbowiki) Ndugu Almano Leonard Mdede amesema kama uongozi wa vyama hivyo wanatoa tamko kwa wanachama wao kuendelea na kazi kama kawaida siku ya septemba mosi ili kuepuka athari zitazoweza kulighalimu taifa na familia zao kwa ujumla.
 
Mwenyekiti wa chama cha Chabbowiki,Ndugu Almano Mdede,katikati akisoma tamko hilo huku akiwa 
amezungukwa na viongozi wenzake na baadhi ya madereva wa Boda boda wa jiji la Dar es salaam.
 

"vyama hivi vya boda boda  vya mkoa vilivyosajiliwa havifungamani na vyama vyovyote vya siasa ila wanachama wake ambao ni wafanyabiashara hiyo ni wanachama wa vyama mbali mbali vya siasa kwa mujibu wa sheria ya Tanzania na sio dhambi kuwa mwanachama wa chama cha siasa na haidhuiliwi na sheria yoyote kuwa mwanachama wa chama cha siasa,sisi viongozi wa vyama hivi vya madereva wa boda boda tunatoa tamko kwa wanachama wa vyama hivyo kwa mkoa huu wa Dar es salaam kuendelea na shughuli zao za kawaida siku ya septemba mosi kwa kufuata kanuni taratibu na sheria za nchi ili kuepuka athari ambazo zitaweza kughalimu taifa na familia zao kwa ujumla ili kulijenga taifa letu"alisema

Nae katibu wa chama cha kiditima,Ndugu Oscar Waluye ameeleza kuwa kanuni za vyama vyao zinazowaongoza katika biashara ya usafilishaji wa abiria kutumia njia za piki piki zina zuio la kushiriki katika shughuli zozote za kisiasa,vyama hivi sio vya kisiasa ila ni vyama vinavyoongoza madereva na kuwasisitiza kufuata kanuni na taratibu za kubeba abiria kama sheria ya Tri ciycle,motorcycle regulation ya machi 2010 inavyoeleza.
 Katibu wa chama cha kiditima,Nugu Oscar waluye katikati akiongea na waandishi wa habari kuhusu kutoshiriki maandamano ya septemba mosi,na kutoa onyo kwa mwanachama yeyote ambaye ataonekana kujiusisha kwa njia yoyote katika maandamano hayo.

"Sisi kana viongozi wa vyama vya waendesha Boda boda kwa namna moja au nyingine hile hatutajishirikisha hata chembe kwa kubeba abiria ambaye amevaa nguo zinazofanana na sare za chama chochote kwa sababu kwa kufanya hivyo tutaonekana tunasafilisha watu wa chama fulani,tunapenda kuuhakikishia umma kwa namna yoyote hile wanachama wanajulikana,vituo vinajulikana,yoyote atakayebainika ameshiriki katika shughuli hiyo atachukuliwa hatua kuanzia ngazi ya kituo,wilaya,mkoa na ikibidi hata ngazi ya taifa."alisema katibu.

Awali mwenyekiti alivitaja vyama hivyo vilivyoshiriki kutoa tamko hilo kuwa ni CHABBOWIKI,KIDITIMA,CHAWAPILA,DABAJA,SEBOA,UMABWILA na UWAPITE.

No comments

Powered by Blogger.