UDO EAST AFRICA KUPELEKA WASHINDI NCHINI SCOTLAND.



Mkurugenzi wa UDO EAST AFRICA,Bw.Ashraf Rwabigimbo akitoa taarifa hiyo mbele ya     waandishi wa habari.

Mtandao wa shirika linaloandaa mashindano ya kucheza duniani linalofahamika kama United Dance Organization lenye makazi yake nchini uingereza limeandaa pambano la kucheza ambapo washindi watapelekwa kushindana na wenzao nchini scotland.
 

Akitoa ufafanuzi huo kwenye ukumbi wa Habari maelezo jijini Dar es salaam,Mkurugenzi wa UDO East Africa Bw.Ashiraf Rwabigimbo amesema shindano hilo lijulikanalo kama Dance Battle Zone linahusisha vijana wenye umri kuanzia miaka 18 na kuendelea na litafanyika kwa awamu mbili ya mkoa na kitaifa, na kwa mkoa huu teyali shindano limekwisha zinduliwa tar 7,august 2016 na kumalizika tar 28,august katika ukumbi wa maisha Basement na mh.joseph haule huku ikibakia mikoa mitatu kwani katika awamu ya mkoa jumla ya mikoa minne tu ndio itakayoshiriki. 

Aliwataja washindi wa pambano hilo kuwa ni kundi la BITZ-HOUSE OF KINETIX ambao wamepata pesa taslimu Tsh.milioni moja,na wa pili ni Nadzz lilbeast,wa tatu ni TAFA Makuzi,wa nne ni Editoo kinywele na mshindi wa tano ni Angeles(Angeles nyigu na Abdully Ally)hawapo pichani ,ambapo washindi wote walipata pesa taslimu na medali za dhahabu na silva,hivyo washindi hao watawakilisha mkoa wa Dar es salaam katika shindano la kitaifa April 2017.


Wakwanza kushoto ni Beston Shabani,wapili ni Amani Hamisi ambao ni washindi toka kundi la BITZ,na anayefuatia ni mkurugenzi wa UDO EAST AFRICA na wamwisho kulia ni Mkurugenzi wa Fedha wa UDO EAST AFRICA Bw.Idris Dossajee wakiwakabidhi mfano wa hundi washindi hao.

Aidha,baada ya kumalizika kwa shindano hilo mkoani hapa sasa litahamia mkoani Dodoma mwezi septemba,Arusha mwezi Octoba na Zanzibar mwezi Disemba mwaka huu ambapo mshindi atawakilisha Tanzania katika mashindano ya UDO World Street Dance Championships yatakayofanyika Glasgow nchini Scotland.
Amani Hamisi ambaye ni mshindi toka kundi la BITZ akionyesha vionjo mbele ya wana habari. 

Vijana wote wenye vipaji na wenye umri uliotajwa na mkurugenzi wanaombwa kujitokeza kuchukua fomu na kushiriki mashindano haya hadhimu ya kucheza kwani kucheza ni kipaji lakini pia ni ajira.

No comments

Powered by Blogger.