POLISI YAUA WAANDAMANAJI ETHIOPIA.



Idadi ya Waethiopia waliouwawa wakati wa makabiliano makali baina ya waandamanaji na maafisa wa polisi katika mji wa kaskazini magharibi mwa Bahir Dar imefikia saba.
Maafisa wa utawala katika mji huo wanasema kuwa takribani watu 7 walipoteza maisha yao katika maandamano hayo yaliyochacha mwishoni mwa juma ingawa Wapigania haki za binadamu wanasema kuwa idadi ya wale waliouawa katika siku tatu za maandamanao ni juu zaidi ya saba waliotajwa na maafisa wa serikali.
 

Waandamanaji hao walikuwa wakipinga sera mpya ya serikali ya kupanua jiji la Addis Ababa ambayo iliwalazimu baadhi yao kupokonywa ardhi hivyo walifunga barabara na kuimba nyimbo zinazopinga utawala ulioko sasa Ethiopia.
Miili ya vijana wawili ilizikwa leo katika eneo hilo na Inaaminika kuwa wawili hao waliuawa na maafisa wa utawala.
 

Kulishuhudiwa pia maandamano makubwa katika eneo la Oromia ambako kunaaminika kuwa watu kadhaa waliuawa ambapo hata hivyo idadi kamili haijulikani.
BBC-imeripoti.

No comments

Powered by Blogger.