MREMA USO KWA USO NA MADEREVA BODA BODA
Mwenyekiti wa Parole Augustino Mrema amewataka madereva bodaboda kote nchini kujiepusha na tabia za kushiriki maandamano ya kisiasa yanayoandaliwa na baadhi ya wanasiasa kwa lengo la kuvunja sheria za nchi.
Pia amewaagiza waendesha bodoboda Kinondoni wampe majina ya polisi wanaowalazimisha kutoa rushwa ili ayakabidhi kwa rais Magufuli.
Mwenyekiti
wa Bodi ya Taifa ya Parole Mhe. Augustine Mrema ( Mwenye Kofia
Katikati) akisisitiza jambo kwa madereva wa pikipiki toka Wilaya ya
kinondoni wakati alipokutana nao ili kusikiliza kero mbalimbali
wanazokutana nazo wakiwa katika kazi zao mapema hii leo jijini Dar es
Salaam.
Mwenyekiti
wa Madereva wa pikpiki Wilaya ya Kinondoni Bw. Almano Mdede akifafanua
jambo kwa madereva pikipiki wa Wilaya ya Kinondoni wa Mwenyekiti wa Bodi
ya Taifa ya Parole Mhe. Augustine Mrema (katikati) alipowatembelea
madereva hao na kusikiliza kero mbalimbali wanazokutana nazo wakiwa
katika kazi zao mapema hii leo jijini Dar es Salaam,kushoto ni Katibu wa
Madereva Pikipiki Wilaya hiyo Bw. George Mbwale.
Baadhi
ya madereva Pikipiki wa Wilaya ya Kinondoni wakimsikiliza Mwenyekiti wa
Bodi ya Taifa ya Parole Mhe. Augustine Mrema (hayupo pichani)
alipokutana nao ili kusikiliza kero mbalimbali wanazokutana nazo wakiwa
katika kazi zao mapema hii leo jijini Dar es Salaam. Picha zote na
Eliphace Marwa -Maelezo. 
Leave a Comment