MOSORE:UJIO WA UKUTA NDIO KIFO CHA UKAWA,MBATIA HANA UTU.
Makamu mwenyekiti wa NCCR- mageuzi Taifa(Bara) amewalipua mbatia na uongozi wa ukawa huku akidai kuwa ujio wa ukuta ndio mwisho wa umoja huo.
Akizungumza na waandishi wa habari leo katika ukumbi wa
habari maelezo jijini Dar es salaam,Bi Leticia mosore amesema hivi sasa kila
chama kinafanya mambo yake kivyake,utakuta CUF wanahangaika kivyao kwenda hadi
The hague kwa madai kuwa wamedhulumiwa katika uchaguzi uliopita,chadema nao
walikuwa wanatoa matamko mbali mbali na sasa wameanzisha operesheni UKUTA na wanakwenda kama Chadema na sio UKAWA, huu
ni mwanzo wa kifo cha UKAWA.
“Ukawa ni kama imepoteza mwelekeo inashindwa kwenda na kasi
ya awamu ya tano ,kiukweli tulihubiri mabadiliko na ukweli Watanzania
tulihitaji mabadiliko,lakini tunashukuru mungu yale yote tuliyokuwa tunayapigia
kelele kuhusu rushwa na ufisadi,uzembe na uzururaji,ukwepaji wa kodi,mafisadi
kutochukuliwa hatua kali na zinazotisha lakini serikali hii chini ya mhe.rais
inafanya kwa vitendo tuliyoyapigia kelele”alisema.
Pia,Bi mosore amezungumzia juu ya hatima ya chama chake cha
NCCR- mageuzi kuwa kwa sasa imevurugwa na haiwezi kufanya siasa ndani wala nje
ya bunge kwa maana mpaka sasa chama chake kimebakia na mbunge mmoja tu na
hakina nguvu kabisa badala ya kujadili hatima ya chama ila Mwenyekiti mbatia
amekuwa mkali kwamba atapigania na kuuenzi UKAWA.
“Hivi sasa NCCR- MAGEUZI imevurugwa haiwezi tena kufanya
siasa sio ndani ya bunge maana amebakia mbunge mmoja tu na hata nje ya Bunge
nguvu zimetuishia kabisa badala ya kujadili wapi tumetoka mafanikio na hasara
za kujiunga na ukawa mwenyekiti Mbatia
amekuwa mkali kweli kwamba atapigania na kuuenzi UKAWA,kimsingi ataupigania
UKAWA ili umsaidie kumuachia jimbo la vunjo lakini sio kwa maslahi mapana ya
chama cha NCCR- MAGEUZI” .alisema makamu.
Aidha,Makamu Mwenyekiti alieleza sababu ya kuitisha mkutano
na waandishi wa Habari kuwa ni kutotambua kusimamishwa kwake kwa uanachama na
uongozi sababu barua aliyopokea haielezi
vifungu vya katiba na kanuni zilizotumika kufikia maamuzi hayo.
.“Nimepata barua iliyoandikwa agast 11,2016 yenye kumb
NA:NCCR M/KM/15/15 inayoeleza kusimamishwa uanachama na uongozi ndani ya
NCCR-mageuzi,Barua hiyo mbali ya kueleza kuwa ni maazimio ya kikao cha julai 16,2016
haielezi sababu ya kunisimamisha uanachama na uongozi wala haielezi vifungu vya
katiba au kanuni zilizotumika kufikia maamuzi hayo halafu inanieleza kama
sikuridhika nikate rufaa katika vikao vya chama”alisema makamu.
Aliendelea
kumzungumzia Mwenyekiti wake Mhe.James mbatia kuwa ana kiuka kanuni na
katiba ya chama lakini Hana utu,kwa
sababu yeye alikuwa akimuuguza mumewe kwa muda mrefu ambaye alifanyiwa
oparesheni julai 28,2016,lakini Mhe.mbatia hakuwai kumpigia simu kujua hali ya
mgonjwa lakini bado aliitisha kikao
julai 16,2016 huku akiweka agenda ya kumjadili yeye na kupanga watu wafikie maamuzi wanayodai
waliyafikia kinyume na katiba na kanuni za chama licha ya yeye kutoa taarifa ya
udhuru kwa Katibu mkuu wa chama ,hivyo ni kukiukwa kwa taratibu,kanuni na
katiba ya chama ya 1992,iliyofanyiwa marekebisho 2014,sura ya kwanza ibara ya
5.
Mwishowe,Makamu mwenyekiti alimaliza kwa Kusema kuwa ameshapatiwa barua rasmi na anatafakari juu ya hatua ya kuchukua ili kudai haki yake huku akiwashauri viongozi wenzake wa UKAWA kuwa wanahitaji kukaa chini kutafakari na kujipanga jinsi ya kufanya siasa za ushindani katika kipindi hiki lakini siasa zinazosaidia Taifa
Leave a Comment