MFUMUKO WA BEI ZA BIDHAA UMEPUNGUA HADI ASILIMIA 5.1.


Image result for ofisi ya takwimu ya taifa
Hali ya Mfumuko wa bei wa bidhaa nyingi hapa nchini umepungua hadi asilimia 5.1 kwa kipimo cha mwaka.
 

Ofisi ya Takwimu imetoa taarifa hiyo juzi jijini Dar es salaam ambapo Mfumuko wa Bei wa Taifa kwa kipimo cha mwaka hua unapima kiwango cha kasi ya Mabadiliko ya bei za bidhaa na huduma zote zinazotumiwa na kaya binafsi katika makundi tofauti ya bidhaa kama Vyakula na vinywaji baridi,vinywaji vyenye kilevi na bidhaa za tumbaku,mavazi ya nguo na viatu,Nishati,maji na makazi,gharama za Afya,usafirishaji n.k.
 

Katika hali hiyo mfumuko wa Bei wa Taifa kwa mwezi julai,2016 umepungua hadi asilimia5.1 kutoka asilimia 5.5 ilivyokuwa mwezi juni,2016.Hii inamanisha kuwa ,kasi ya upandaji wa Bei za bidhaa na huduma kwa mwaka ulioisha mwezi julai,2016 imepungua ikilinganishwa na kasi iliyokuwepo kwa mwaka ulioisha mwezi juni,2016.
 

Aidha,taarifa hiyo imeonyesha kuwa mfumuko wa bei kwa bidhaa za vyakula na zisizo za vyakula kwa kipimo cha mwaka wa bidhaa za vyakula nyumbani na migahawani umepungua hadi asilimia 7.8 mwezi julai,2016 kutoka asilimia 8.3 mwezi juni,2016,huku mfumuko wa Bei  wa Bidhaa na huduma zote isipokuwa Bidhaa za Vyakula na Nishati kwa mwezi julai,2016 umepungua hadi asilimia 2.6 kutoka 3.0 ilivyokuwa juni,2016.
 

Japokuwa kumekuwa na punguzo kubwa la mfumuko wa Bei kwa kipimo cha mwaka lakini kuna ongezeko kidogo la asilimia 0.03 kwa mwezi julai 2016,unaopimwa kwa kipimo cha mwezi.
 

Mkurugenzi mkuu,
ofisi ya Taifa ya Takwimu.

No comments

Powered by Blogger.