MAKONDA:HATUNA TATIZO LA AJIRA ILA TATIZO LA FIKRA.

Image result for MAKONDA
Mheshimiwa mkuu wa mkoa wa Dar es salaam amesema mkoa wake na nchi kwa ujumla hakuna tatizo la ajira ila tatizo la fikra.

Akizungumza jana kupitia kipindi cha Terminal kinachorushwa na kituo cha clouds Fm,Makonda amesema mkoa wake hauna tatizo la ajira ila tatizo la fikra kwa sababu kuna watu wanatoka nje na kuja hapa wanatengeneza pesa na wanaondoka huku wanamuacha mzawa yupo vile vile,sasa tatizo ni la ajira au fikra.

"Dar es salaam na Tanzania yote hakuna tatizo la ajira ila tazizo ni fikra"alisema.

Aliendelea zaidi na kutolea mfano nchi zilizoendelea kuwa hata zenyewe hakuna siku wanaita wananchi wao na kuwambia leo tunatoa ajira ila ni juhudi za kuchangamkia fursa,lakini anashangazwa na baadhi ya wasomi ambao wanasubiri waletewe kila kitu na ndio maana kila siku wanazunguka na baasha kutafuta kazi na wakati kuna vitu vingi vya kufanya kwani sehemu yoyote yenye changamoto kuna fursa.

No comments

Powered by Blogger.