WANANDOA WAUAWA KIKATILI KISA DENI LA BISKUTI NCHINI INDIA.

Image result for Dalit

Mtu mmoja na mkewe kutoka jamii ya Dalit inayobaguliwa tangu jadi nchini India wameuawa, mmoja akiwa amekatwa kichwa na mwengine kunyongwa kwa kushindwa kulipa deni la Rupee kumi na tano ambayo ni karibu senti ishirini na mbili tu,BBC Swahili imeripoti,,,,,,

Polisi kaskazini mwa taifa hilo wamethibitisha kisa hicho ambapo yasemekana mfanyabiashara anayetokea jamii ya hadhi ya juu,aliwaua wanandoa hao kwa kushindwa kulipa deni la biskuti walizokuwa wamewachukulia watoto wao.

Ubaguzi kwa misingi ya kijamii umeenea sana nchini India, huku watu wa jamii ya Dalit waliokuwa wamebandikwa jina la 'the untouchables' wakiwekwa kwenye daraja la chini kabisa kwenye sera hiyo ya kibaguzi nchini India iitwayo 'caste' ambapo wananyimwa fursa nyingi za kimaendeleo na hivyo kubaki katika wimbi la umaskini .

Hata hivyo Visa vya ukatili wa kibaguzi dhidi ya jamii ya Dalit katika jimbo la Gujarat vimeongezeka mnamo siku za hivi karibuni na vimesababisha wimbi la maandamano kutoka watu wa jamii hiyo.

No comments

Powered by Blogger.