ASKARI ALIYEMUUA MWANGOSI AFUNGWA MIAKA 15 JELA.
Askari wa kikosi cha kutuliza ghasia (FFU) mwenye namba G .2573 Pacificius Cleophace Simon (27)
MAHAKAMA kuu ya Tanzania kanda ya Iringa leo imemuhukumu kwenda jela miaka 15 kwa kosa la mauaji ya bila kukusudia askari wa kikosi cha kutuliza ghasia (FFU) mwenye namba G .2573 Pacificius Cleophace Simon (27) aliyemuua mwandishi wa habari wa kituo cha Chanel Ten Daudi Mwangosi.
Maamuzi hayo yametolewa leo baada ya kesi hiyo kuahirishwa juzi na Jaji Paul kihwelo ambaye alipitia utetezi wa mshitakiwa na maoni ya Wazee wa Baraza,ambapo mshtakiwa huyo alitiwa hatiani kwa kosa la kuua bila kukusudia na hukumu yake ingetolewa leo.
Leave a Comment