Wednesday, August 24, 2016

IDADI YA WALIOKUFA KATIKA TETEMEKO LA ARDHI NCHINI ITALIA YAFIKIA 120.


Image result for EARTHQUAKE IN ITALY
Mpaka sasa watu 120 wamekufa na wengine 368 kujeruhiwa katika tetemeko la ardhi eneo la milima ya Italia ya kati, alasiri Waziri mkuu wa Italy Matteo Renzi amesema.
 

Idadi hiyo ni tofauti na hile ya awali ambayo inaeleza takribani watu 73 walifariki kutokana na tetemeko hilo la ardhi.
 

Tetemeko lenye nguvu 6.2 kwa kipimo cha richter limetokea nyakati za 3:36 (1:36 GMT), 100km (65 miles) kaskazini-mashariki mwa Roma, si mbali na Perugia.

Watu themanini na sita wamekufa ambao walikuwa katika mji wa kihistoria wa Amatrice, ambapo Meya alisema robo tatu ya Mji umeharibiwa na uharibifu mwingine ukitokea nchi jirani ya Accumoli.

Watu wengi bado wanaaminika kuwa wamefukiwa chini ya kifusi huku vikosi vya uokoaji vikitumia vifaa vizito na mikono yao kuondoa vifusi ili kutafuta kama kuna miili mingine ambayo imefukiwa.

Taarifa zingine zinaeleza kuwa msichana wa miaka 8 aliokolewa akiwa hai katika kijiji cha Pescara del Tronto baada ya kunaswa chini kwa masaa 17.

Mr Renzi alitoa shukrani kwa waliojitolea kuokoa majeruhi huku akiahidi "hakuna familia, hakuna mji, hakuna kitongoji kitacho achwa nyuma".


BBC imeripoti.

No comments:

Post a Comment