Thursday, August 25, 2016

BIRDMAN ATAKA KUMALIZA BIFU YAKE NA WAYNE.


Image result for lil wayne news
Kufatia bifu kali iliyopo kati ya wasanii wawili marafiki wakubwa ambao wengi tunafahamu kama baba na mwana yaani Birdman na Lil Wayne,hatimaye Birdman amesema anataka kurudisha mahusiano yao kama ilivyokuwa awali.

Bifu inayoendelea kati Lil Wayne na studio yake ya Cash Money, na hasa zaidi mmiliki wake Birdman ambaye ameonekana kwenye mahojiano na ESPN Cari champion's na kuzungumza juu ya uhusiano wake na Weezy huku akitangaza kwamba anatarajia kufanya mambo ya haki na rafiki yake wa zamani.

Hasa Birdman anasema anataka kurudisha uhusiano wake na wayne kwani anaamini kwamba Wayne bado ni mtoto wake na lebo ya Cash Money bado inaendelea.

"Dhahiri sijapenda juu ya mambo mengi aliyosema, lakini mwisho wa siku mimi katika maisha yangu sijawahi kusema baya lolote juu yake.Birdman alisema.

Hata hivyo Birdman ametangaza kuwa "Hatomaliza gemu ya muziki bila Wayne," hivyo kuna matumaini kuwa bifu yao yaweza kumalizwa siku za hivi karibuni.


No comments:

Post a Comment