Thursday, September 15, 2016

GAVANA BOT ASHAURI JUU YA KILIMO KUONGEZA PATO LA TAIFA.


Image result for benno ndulu
Gavana wa Benki kuu ya Tanzania(BOT) ameshauri kuongezwa kwa tija na thamani kwenye kilimo ili kiweze kunyanyua zaidi uchumi wa nchi kwa kuongeza pato la taifa.

Profesa Benno ndulu amesema hayo jana wakati akizungumza na waandishi wa habari katika ukumbi wa benki kuu jijini Dar es salaam wakati akitoa taarifa kuhusu hali ya uchumi wa Tanzania kupitia sekta mbali mbali ambazo zinachangia pato la taifa.

Gavana amesema kwa sasa kilimo kimepungua katika kuingiza mapato ya taifa kutoka 50% katika kipindi cha nyuma hadi sasa kwa 25% na katika fedha za kigeni kilimo kupitia mazao makuu yote sita kwa pamoja yanachangia chini ya 9% ya mapato yote ya fedha za kigeni ukilinganisha na zamani ambapo kilimo kilikuwa kinachangia kwa 70% ya mapato ya fedha za kigeni na hii ni kutokana na changamoto za teknolojia ya uhifadhi mazao na kushuka kwa thamani ya mazao katika kilimo.

"Ni kweli yakuwa bila kilimo kukua kwa kasi hata uchumi hauwezi kukua kwa kasi kwa kuwa kilimo ni sehemu kubwa sana ya uchumi,kwa sasa kilimo kinachangia 25% na sio 50% kama ilivyokuwa awali kwa sababu ya changamoto nyingi zikiwemo za teknolojia na thamani"alisema.

Aidha Prof..Ndulu alizitaja sekta zinazoongoza kwa kuingiza mapato ya kigeni kwa sasa kuwa ni utalii inayoongoza kwa kuingiza dola bilion 2.5,pili viwanda dola bilioni 1.5,tatu ni dhahabu inayoingiza dola billioni 1 na millioni 200,shughuli za usafilishaji biashara kwenda nchi jirani dola bilioni 1.1 na kilimo ni ya tano inayoingiza dola millioni 850 kwa mazao yote makubwa kwa pamoja.

Aliendelea kusema kuwa ni dhahiri kwamba hali ya uchumi wa Tanzania ni nzuri na inatoa matumaini makubwa kwamba shughuli halali za kiuchumi zinaendelea kutekelezwa kama ilivyotarajiwa hapo awali hivyo lengo la ukuaji wa pato la Taifa la 7.2% kwa mwaka 2016 litafanikiwa kwa sababu hali ya makusanyo ya mapato inaridhisha.

Hata hivyo alimalizia kwa kusema kuwa uwiano wa makusanyo ya mapato na uongezekaji wa deni la taifa kitaalamu unaimilika ukizingatia mwaka huu wa fedha ulioishia juni takribani trilioni 13.5 zilikusanywa na deni la taifa alizidi dola bilioni 21 hivyo bado mwenendo wa uchumi unaendelea vizuri.

No comments:

Post a Comment