Tuesday, August 2, 2016

TUNDU LISSU AKANA MASHTAKA MAHAKAMANI NA KUSEMA HAYA...


Mhe.Tundu lissu amekana mashtaka yanayomkabili ya kutoa maneno ya uchochezi dhidi ya Mhe.Rais wa jamuhuri ya muungano wa Tanzania.

Akisomewa mashtaka katika hatua ya awali leo mbele ya hakimu Mkeya wa mahakama ya hakimu mkazi kisutu jijini Dar es salaam,kuwa alitoa maneno hayo mnamo juni 28,mwaka huu,mh.Lissu alikana mashtaka hayo hivyo kesi kupangwa kusikilizwa Agosti 24,mwaka huu.
Wakati akitoka nje ya mahakama,Mh.Lissu aliweza kuongea na wanahabari kuhusiana na mustakabali wa kesi hiyo huku akieleza kuwa wameshindwa hata kuandika alichokisema.
 

"Waendesha mashtaka wameshindwa hata kuandika nilichokisema maana wamekosea sentensi wanayodai ni uchochezi"alisema. 

Aidha Mhe.lissu alikwenda zaidi na kuzungumzia masuala ya mikutano ya hadhara na maandamano huku akidai kuwa kama chama kilichopata usajili wa kudumu kina haki ya kufanya mikutano hiyo na maandamano na Rais hana mamlaka ya kuzungumzia isipokuwa ni OCD pekee.

"Sheria ya Tanzania inasema chama kilichopata usajili wa kudumu kina haki ya kufanya mikutano ya hadhara na maandamo mahala popote sio kwenye makambi ya jeshi au makambi ya polisi lakini mahala pengine popote ukiwa na usajili wa kudumu kama chama cha siasa una haki ya kufanya mikutano,sasa kina mrema wasiokuwa na mbunge wala diwani wakafanye wapi mikutano?na wakina cheyo na wale wengine wenzao wale wao wakafanye mikutano wapi na wakati hawana hata mwenyekiti wa kitongoji"Lissu alisema.

Pia,Mhe.Lissu alisisitiza juu ya suala la haki ya kufanya mikutano ya hadhara huku akidai kauli za kwamba mkafanye mikutano mahali mlipochaguliwa ni za mtu asiyesoma sheria.
"Hizi kauli za kwamba mkafanye mikutano katika mahali mlipochaguliwa ni za mtu anayefikiria na wala asomi sheria ila anafikiria kila linalomjia kichwani mwake ndio sheria na huo ndio udikteta tunao ukataa na tutaendelea kuukataa"Lissu alisema.
 

Aliendelea,kuzungumzia masuala ya kisheria huku akigusia moja ya mamlaka ya Rais wa jamhuri wa muungano huku akisema sio kazi yake kuzungumzia masuala ya mikutano ya hadhra ya vyama vya kisiasa.
 

"Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania,kwa mujibu wa katiba ya nchi hii na sheria zake zote,hana mamlaka yoyote,ya kusema lolote au kufanya lolote kuhusiana na mikutano ya hadhara,sio kazi yake,Kwa mujibu wa sheria ni kazi ya OCD"Lissu alisema.

Mwishoni mhe.Lissu alisistiza suala la kufanya mikutano ya hadhara na maandamano nchi nzima sio kwa sababu wamefungua kesi tu ila wana haki kisheria.

No comments:

Post a Comment