Msanii wa nyimbo za Gospel nchini Goodluck Gozbert amesema kazi yake sio uandishi wa nyimbo licha ya kuandika nyimbo nyingi na kuimbwa na wasanii wengine.
Goodluck amesema hayo wakati akifanyiwa mahojiano katika kipindi kimoja cha radio kinachorushwa na radio kubwa hapa nchini.
Akifafanua kauli yake hiyo ya kuwa yeye sio mwandishi,Goodluck amesema wale wote aliowaandikia ni marafiki zake ana connection nao na wanaishi kama familia katika maisha yao ya kila siku hivyo uhisi kama wanafanya mazoezi.
"Uandishi sio kazi yangu yaani huwezi nipigia simu tu goodluck naomba tufanye kazi nitakulipa kiasi fulani na huwezi nisikia nimefanya hivyo kwa sababu ninachoandika kina mahusiano makubwa na jamii lakini pili kina mahusiano na nichoamini mimi kiimani uweza kinaweza nitokea,mimi ni Gosper artist kwaiyo wimbo kama moyo mashine au nenda kamwambie ni vitu vinavyotokea kwenye jamii na ni hatua kabla ya kufikia maisha ya ndoa"alisema.
Aidha Goodluck ameweka wazi kuwa hayupo kwenye mahusiano yoyote ya kimapenzi na swala la kuoa anasubiri mpaka muda utakapofika na kumtambua mtu sahihi kwake,licha ya kuwa anasumbuliwa na wanawake kwenye simu mara kadhaa.
Goodluck ni msanii wa Gosper anayetamba na nyimbo kama" ipo siku yangu" na "Acha waambiane"amekuwa akiwaandikia wasanii wengine wa Bongo fleva kama Ben pol wimbo wa "Moyo Mashine",Barraka Da Prince"Siachani nae"na "nivumilie"pia Mo music wimbo wa "Basi nenda".
No comments:
Post a Comment