Tuesday, July 26, 2016

TAMASHA KUBWA LA UTAMADUNI KUFANYIKA DAR.

Tamasha kubwa la utamaduni lililopewa jina la DAR FESTIVAL linatarajiwa kufanyika mwaka huu jijini Dar es Salaam.

Akitoa taarifa hiyo katika ukumbi wa habari maelezo,Mratibu wa Tamasha hilo Bw.Farid Faraji amesema wanatarajia kufanya tamasha hilo kubwa la kimapinduzi mwezi wa 9 ambalo litahusisha michezo,Burudani na shughuli mbali mbali za kitamaduni za ndani ya nchi yetu.

"Mwaka huu tamasha ndo linaanza na litakuwa la kimapinduzi na tutaliboresha ili liwe la kimataifa"alisema mratibu.

Aidha,alizitaja baadhi ya faida za tamasha hilo ikiwemo la ukusanyaji wa mapato ambapo katika kipindi hiki ambacho nchi yetu ipo katika wakati wa kukusanya mapato basi kupitia tamasha hili ambalo litatangaza utamaduni litaweza kusaidia serikali kupata mapato kupitia utalii. 
"Tamasha hili pia litaweza kuisaidia serikali kupata mapato,tukiitangaza Tanzania tutakuwa tumetangaza utalii hivyo sekta hii itakuwa chanya zaidi katika kuingiza mapato"alisema

Pia,Diwani wa kata ya Ilala ambaye ni mlezi wa kamati ya DAR FESTIVAL Mhe.Saady Khimji,ametumia fursa hiyo kuwapongeza vijana kwa kuamua kumteua kuwa mlezi wa kamati sababu madiwani wapo wengi lakini yeye ndio amepewa nafasi hiyo hivyo ametoa wito kwa viongozi hasa wa wizara ya habari utamaduni na michezo kuhakikisha wanasaidia kufanikisha Tamasha hilo,bila kusahau wadau wanapaswa kujitokeza kudhamini Tamasha hilo kubwa la kimapinduzi.
"Haitakuwa na faida ya kuwa mlezi halafu ukashindwa kusimamia jambo hili na lishindwe kufanikiwa,hivyo nitoe wito kwa viongozi mbali mbali hasa wizara yetu ya Habari,Sanaa,utamaduni na michezo inayoongozwa na Mhe.Nape Nnauye na wadhamini kuhakikisha wanatusaidia ili kufanikisha Tamasha hili"alisema

Tamasha hili linatarajiwa kufanyika kwa mara ya kwanza jijini Dar es salaam ambapo uzinduzi wake utafanyika Viwanja vya Leaders club ili kuwavutia watu kujitokeza kushuhudia kabla ya kuhamia Makumbusho kwa siku ya pili.

No comments:

Post a Comment