Thursday, July 28, 2016

OLD GUARDS BASKETBALL KUJA NA BONANZA LA UZALENDO.

Klabu ya wachezaji wa mpira wa kikapu wa zamani maarufu kama Old Guards Basketball imeandaa Bonanza linalojulikana kama bonanza la uzalendo litakalofanyika siku ya jumapili katika viwanja vya Ghymkhana jijini Dar es Salaam.

Bonanza hilo amabalo litashirikisha timu zingine za mpira wa kikapu za wachezaji wa zamani kama Chango'mbe veterans,Dodoma veterans,Pazi veterans na UDSM veterans maarufu kama LIBENEKE linatarajiwa kufanyika siku hiyo kuanzia saa 3 mpaka 10 jioni ambapo timu hiyo itakuwa inatimiza miaka 18 tangu kuanzishwa  kwake.
 

Aidha,mbali na kuwepo kwa mechi za watu wazima,pia kutakua na mechi za watoto chini ya miaka 14 ambao wanafundishwa katika programu ya Mambo Basketball kila jumapili kuanzia Saa 4 hadi 7 mchana katika viwanja hivyo vya ghymkhana ikiwa na lengo la kurithisha watoto kuwa na mapenzi ya mchezo huu maarufu duniani.

Mwenyekiti wa klabu hiyo Bw.Lawrence Cheyo aakieleza nia ya kufanya bonanza hilo la Uzalendo kuwa ni kuhamasisha mazoezi ya kiafya,kuboresha na kuimarisha ushirikiano kati yao na kukumbushana mazoea ya kupima Afya mara kwa mara.
 

Sambamba na hilo kutakuwa  na zoezi la upimaji wa Afya kwa magonjwa kama presha,kisukari na mengine,lengo ni kujua Afya na kudhibiti mapema endapo kuna mtu atagundulika  ana kasoro.
Katibu wa klabu hiyo Bw.Juma Akilimali akielezea kuhusu kuwaalika watoto wanaoishi katika mazingira magumu kutoka kituo cha Malaika cha Kinondoni kushiriki katika bonanza hilo ambapo watacheza na watoto wenzao michezo mbali,sambamba na kuwapa zawadi kwajili ya kuboresha huduma katika kituo hicho.
Hata hivyo,Katibu ametoa shukrani kwa wadhamini wa Bonanza hilo ambao ni East Africa Radio na CRDB Bank,huku akizitaja zawadi za washindi kuwa ni Kombe,Cheti cha ushiriki na posho ya nauli.

Mkuu wa vipindi wa East Africa Radio Bw.Nasser Kingu akieleza sababu ya kituo hicho kudhamini Bonanza hilo kuwa ni kuthamini michezo kwa wana Africa Mashariki sababu wanajua michezo ni Afya na ni muhimu kuwekeza katika hilo.
 

Old guard Basketball wamekuwa wakiandaa Bonanza kila mwaka tangu kuanzaishwa kwake mwaka 1998 na Baraza la michezo la Taifa (BMT) na wamekuwa wakizunguka mikoa mbali mbali kama Tanga,Mombasa na Zanzibar,hivyo wanatoa wito kwa wapenzi na wachezaji wa mchezo huu kujitokeza siku hiyo.

No comments:

Post a Comment