Wednesday, July 27, 2016

"NILIKUWA MBUNGE KABLA SIJAINGIA BUNGENI" PROFESSOR JAY.





Mheshimiwa Joseph Haule a.k.a Prof.Jay ambaye ni mbunge wa mikumi mkoani Morogoro amesema alikuwa mbunge kabla ya kuingia bungeni kwa sababu yeye alikuwa "mbunge wa kitaa" kupitia mziki wake ambao ulikuwa unawakilisha watu na ndio maana alikuwa na mashabiki hadi kwa waheshimiwa wabunge.

Mhe. Haule amezungumza hayo leo pindi alipokuwa anatambulisha single yake mpya ya "Kazi Kazi" aliyofanya na mwanamziki wa singeli nchini sholo mwamba chini ya produza Mesen selekta katika kituo cha radio cha Clouds Fm jijini Dar es Salaam.

Aidha,ameeleza sababu za yeye kufanya mziki wenye maadhi ya singeli kuwa mziki huu una utambulisho wa nyumbani na Tanzania ilikuwa na changamoto ya kupata mziki kama huu.

"mziki huu una identity ya watu wa Tanzania na kumekuwa na changamoto ya kuwa na muziki wa nyumbani,sasa kwenye muziki huu kuna chakacha,mdundiko,mdumange na midundo mingine lakini mziki huu haukupewa sapoti na mimi nilikuwa na hamu ya kufanya kitu kama hiki chenye mchanganyiko na hip hop"alisema muheshimiwa.

Aliendelea kusema sababu zingine za kufanya mziki huu kuwa ni kuunyanyua kwani unapendwa na vijana wengi na wanaofanya wamechoka na kukata tamaa hivyo kushilikiana nao ni kusapoti na kuupeleka katika kiwango cha juu kwani umekosa sapoti inayotakiwa.








No comments:

Post a Comment