Wednesday, July 27, 2016

MUGABE AWAONYA MASHUJAA WASALITI.



Rais wa Zimbabwe Robert Mugabe amewatahadharisha mashujaa wa vita vya uhuru ambao wameonya kuwa huenda wakakataa kuunga mkono serikali yake kufuatia mporomoko mkubwa zaidi wa uchumi kuwahi kushuhudiwa nchini humo.

 Rais Mugabe aliwaonya mashujaa hao alipokuwa akihutubia umati wa wafuasi wa chama tawala cha Zanu-PF.

 Aidha rais huyo aliwataka viongozi wa chama cha mashujaa kuwachagua viongozi wapya kwani viongozi wa mashujaa hao wa vita vya ukombozi kutoka mikononi mwa wakoloni walikuwa wameshawishiwa na mataifa ya magharibi.

Mashujaa hao walioongoza uvamizi wa mashamba ya wazungu mwaka wa 2000,wameonya kuwa watakataa kumuunga mkono mugabe endapo hataweka mikakati ya kukomesha ubadhirifu wa mali za umma na ufisadi uliokithiri mipaka na kusababisha maandamano makubwa zaidi.

Mugabe ameonya kuwa wale ambao wanaendeleza maandamano yaliyoshuhudiwa katika siku za hivi karibuni huenda wakafungwa jela kwani taifa hilo halina haja ya mapigano ya wenyewe kwa wenyewe.

Hata hivyo,Rais mugabe mwenye umri wa miaka 92 ameahidi kuwania awamu mpya ya utawala katika uchaguzi wa mwaka wa 2018,huku baadhi ya viongozi wa chama cha chake wakiwa wameanza kung'ang'ania madaraka.
 Source-BBC swahili.





No comments:

Post a Comment