TRL YAFANYA MABADILIKO YA RATIBA YA SAFARI ZA ABIRIA KWENDA BARA.

Image result for kampuni ya reli


Uongozi wa kampuni ya reli Tanzania(TRL) umeamua kuongeza safari ya tatu ya treni ya abiria ya kawaida kwenda bara ambayo itaondoka Dar es salaam kila jumapili,na safari ya kwanza itakuwa septema 4,2016 saa 9 alasiri.

Treni hiyo ya huduma ya kawaida itakuwa na mabehewa 8 ya daraja la 3,mawili dalaja la pili na mawili daraja la kwanza, katika stesheni za morogoro na Dodoma yataongezwa mabehewa 2 ya dalaja la 3.

Aidha treni ya Deluxe imebadilishwa siku ya kuondoka badala ya jumapili kwa sasa,kuanzia septemba 2016,itakuwa inaondoka siku ya alhamisi saa 2 asubuhi kutoka Dar es salaam.
Hali kadhalika mabadiliko hayo pia yataongeza safari za treni ya kwenda mpanda kutoka Tabora badala ya 2 za sasa zitakuwa 3 kwa wiki  ambazo ni jumatatu,jumatano na jumamosi.

Wakati huo huo uongozi wa TRL umefanya uamuzi wa kihistoria wa kupeleka huduma ya kuuzwa kwa tiketi za safari yake mjini kasulu ambapo kuanzia septemba mosi itafungua kituo cha reli ambacho kitafanya kazi ya kutoa huduma hiyo kwa wasafiri wanaotoka kasulu mjini na maeneo jirani.kwa uamuzi huo TRL imetoa nafasi za tiketi za behewa moja la dalaja la 3 mpango pia uko mbioni wa kufungua kituo kama hicho siku zijazo mjini kibondo hali itakaporuhusu kulingana na mahitaji halisi ya abiria.
Taarifa imesisitiza kuwataka wasafiri na wananchi kwa ujumla nchini hususani wale wa mpanda na kibondo kutumia fursa ya kuongezewa safari ya huduma kuletewa bkaribu kwa kufuata sheria,taratibu na kanuni ili hatua iliyochukuliwa na TRL iwe na tija iliyokusudiwa.

Aidha taarifa zaidi zinaarifu kuwa hatimaye TRL imefanikiwa kuongeza mabehewa mawili zaidi  ya treni ya pugu na kufikia idadi ya behewa 18 hadi jana Agosti 22,2016.Ni matarajio ya uongozi ifikapo Agosti31,2016 treni hiyo ya jiji itakuwa na mabehewa 20 iloahidi ili kupunguza msongamano unaosababishwa na abiria kuwa wengi katika safari mbili za awali katika awamu zote 2 ya asubuhi na jioni.

imetolewa na Ofisi ya Uhusiano kwa Niaba ya 
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TRL,
Nd,Focus makoye sahani,
Dae r es salaam,
Agosti 23,2016.

No comments

Powered by Blogger.