KWA MARA NYINGINE RONALDO ATAJWA KAMA MCHEZAJI BORA WA UEFA.


 Image result for ronaldo 7 2015
Cristiano Ronaldo ametajwa kama Mchezaji Bora wa uefa barani Ulaya kwa mara ya pili baada ya kushinda Ligi ya Mabingwa na Euro 2016 msimu uliopita.

Nyota huyo wa Real Madrid amempiku mchezaji mwenzake Gareth Bale na mshambuliaji wa Atletico Madrid Antoine Griezmann katika kura zote zilizopigwa.

Ronaldo mwenye umri wa miaka 31, alifunga penalti ya ushindi kwa Real madrid katika fainali ya Ligi ya Mabingwa dhidi ya Atletico na nahodha huyo wa Ureno kuipa ushindi timu yake,hali kadhalika kuipatia ushindi timu yake ya taifa katika mashindano ya Euro 2016 mwezi Julai.
 

Hiyo ni rekodi nzuri ambayo Ronaldo anazidi kujiwekea katika historia ya maisha yake ya soka ukiachana na rekodi nyingi ambazo amekwisha weka.

No comments

Powered by Blogger.