KOREA KASKAZINI IMEFYATUA KOMBORA LINGINE HADI BAHARI YA JAPAN.
Jeshi la Marekani limesema liliweza kufuatilia kombora hilo lililopaa hadi umbali wa kilomita mia tangu na kabla ya kuanguka katika Bahari ya Japan.
Kurushwa kwa kombora hilo kumefanyika huku mawaziri wa mambo ya nje kutoka Japan, China na Korea Kusini wakiendelea na mkutano wao mjini Tokyo.
Waziri mkuu wa Japan Shinzo Abe ameelezea kitendo cha Korea Kaskazini kuwa kisichoweza kukubalina na kwamba ni tishio kwa usalama wa taifa lake.
Awali, Korea Kaskazini ilikuwa imeonya kuwa mazoezi ya kijeshi yanayoendelea kwa sasa kati ya wanajeshi wa Marekani na Korea Kusini yanaongeza hatari ya kuzuka vita rasi ya Korea.
Mazoezi hayo ambayo yamepewa jina Ulchi Freedom yanashirikisha wanajeshi 80,000 wa Marekani na Korea Kusini na ni mwigo wa jinsi ya kujikinga dhidi ya uvamizi dhahania kutoka kwa Korea Kaskazini.
Korea Kaskazini imepigwa marufuku na UN kutumia teknolojia ya makombora marefu na nyuklia.
Lakini miezi ya karibuni, imerusha makombora kadha na inaaminika kukaribia kufanya jaribio la tano la bomu la nyuklia.
BBC imeripoti.
Leave a Comment