JPM AFANYA UTEUZI IDARA YA USALAMA WA TAIFA.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amemteua Dkt. Modestus Francis Kipilimba kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Usalama wa Taifa, Kabla ya uteuzi huo Dkt. Modestus Francis Kipilimba alikuwa Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA).
Dkt.
Modestus Francis Kipilimba anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Rashid
Othman ambaye amestaafu. Dkt. Modestus Francis Kipilimba ataapishwa leo
mchana tarehe 24 Agosti, 2016 Ikulu Jijini Dar es Salaam. Aidha, Rais
Magufuli amemteua Robert Msalika kuwa Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya
Usalama wa Taifa.
Kabla ya
uteuzi huo Robert Msalika alikuwa Afisa Ubalozi katika Ubalozi wa
Tanzania nchini Ethiopia. Wakati huo huo, Rais Magufuli amemteua
aliyekuwa Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Usalama wa Taifa George
Madafa kuwa Balozi na nchi atakayopangiwa itatajwa baadaye. Wakurugenzi
na Naibu Wakurugenzi wa Idara ya Usalama wa Taifa waliopo wanaendelea na
nafasi zao.
Leave a Comment